Skip to main content

MAADHIMISHO YA WIKI YA USAFIRI WA ANGA DUNIANITanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya usafiri wa anga, (International Civil Aviation Day) ambayo huadhimishwa Desemba 7 kila mwaka. Lengo la maadhimisho hayo ni kukuza uewelewa wa wananchi kuhusu sekta ya usafiri wa anga na namna inavyochangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mataifa mbalimbali.

Mwaka huu siku hiyo inaadhimishwa ikiwa ni miaka sabini (70) tangu kupitishwa na kusainiwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga (maarufu kama Chicago Convention) na tangu kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).  

Kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni “Miongo Saba ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Usafiri wa Anga na Kusherehekea Miaka Sabini ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago”.

Kwa Kiingreza: “Celebrating Seven Decades of Cooperative of Air Transport Progress and Celebrating 70 years of Chicago Convections.”

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kushirikiana na wadau wa sekta wameandaa shughuli mbali mbali kuadhimisha miaka sabini ya usafiri wa anga duniani.  Kwa vile tarehe 7 Desemba ni siku ya Jumapili, maadhimisho yetu yatafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Desemba.

Moja ya Shughuli zitakazofanyika katika kipindi cha maadhimisho ni maonyesho ya wadau wa usafiri wa anga kwa siku tatu, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Desemba katika viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Banana- Ukonga.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba, anatarajiwa kuwa mgeni ramsi katika  maonyesho hayo yanayolenga kutangaza shughuli za wadau wa sekta ya usafiri wa anga. Wadau hao ni pamoja na vyuo vya usafiri wa anga, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, makampuni ya ndege, Mdhibiti wa sekta na wadau wengine wanaotoa huduma kwenye viwanja vya ndege wakiwemo Swissport na Equity Aviation.

Tarehe 4 Desemba kutakuwa na kongamano la wadau wa sekta, litakaloongozwa na kauli mbiu “Miaka 70 ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga- Mikakati ya Tanzania Katika Kuimarisha Maendeleo ya Usafiri wa Anga”. Pamoja na mambo mengine kongamano litaangalia mbinu za kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini, mchango wake katika kukuza uchumi, kinga ya abiria dhidi ya majanga, mchango ya huduma ya hali ya hewa kwenye usafiri wa anga pamoja na changamoto  zinazokabili sekta hii. Kongamano litafanyikia ukumbi wa mikutano, Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga na kufunguliwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dr. JUma Malik Akil.

Katika maadhimisho haya, pia kutakuwa na safari maalum ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa kundi la watoto 20 wakiwemo wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo na wale wa kundi la mazingira maalum. Safari imelenga kuchochea udadisi wa watoto kwenye sekta ya usafiri wa anga na kuwaamasisha ili wasome zaidi na hatimae kuja kutumikia sekta ya usafiri wa anga.

Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dr. Harrison Mwakyembe, ambaye atakuwa Mgeni Rasmi siku ya kilele cha maadhimisho, tarehe 5 Desemba, atatembelea na kukagua maendeleo ya baadhi ya miradi katika sekta ya usafiri wa anga. Miradi atakayoikagua ni pamoja na Mradi wa Swissport unaohusisha ujenzi wa Bohari Maalumu la mizigo inayosafirishwa na usafiri wa anga ambayo ina uwezo wa kutunza wanyama hai. Tanzania kwa mara ya kwanza itakua na huduma za kuhifadhi wanyama hai wanaosubiri kusafirishwa au kupokelewa kupitia usafiri wa anga. Mh Waziri pia atapata nafasi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jumba la Abiria (Terminal 3) katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere. Aidha, Mh. Waziri atazindua Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania- TCAA, yaani Aviation House.

Kamati ya wadau ya maandalizi inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria kwenye maonyesho na kutumia fursa hiyo kujifunza zaidi kuhusu sekta ya  usafiri wa anga na mchango wake katika maendeleo ya huduma na uchumi wa nchi yetu. Makampuni ya ndege yanatarajiwa pia kuchukua nafasi hiyo kutoa huduma zao za tiketi wakati wa maonyesho. 

Comments

Most Viewed Posts

Job Opportunities at Air Tanzania (ATCL)

VACANCIES ANNOUNCEMENT Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet. The Company is therefore inviting applications from qualified personnel to fill various positions. 1.      POSITIONS:  1.1. Dash 8 – Q400 Mechanical and Avionics Certifying Engineers (6 POSTS)     a)    Qualifications·         ·          Must possess a valid Aircraft Maintenance Engineers License (ICAO TYPE II).  ·         ·          Must possess a valid Dash 8 – Q400 Approval/License. ·      Must have successfully completed Dash 8 – Q400 type course from an Approved Training Organisation.        ·       Must have Aircraft Maintenance working experience, as a certifying engineer, of not less than 5 years; 2 of which being on Dash 8 – Q400. Experience must include release to service certification after “A” Check and above.        ·          Computer literacy·         ·          Fluency in English·        

Job Opportunities at Air Tanzania: Pilots-in-Command, Co-Pilots,Aircraft Maintenance Engineers and Cabin Crews.

Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet. The Company is therefore inviting application from qualified personnel to fill various positions. 1. POSITIONS: 1.1  Pilot-in-Command – Dash 8 (11 Posts) a) Qualifications: Must possess Airline Transport Pilot License (ATPL) and with performance “A”.Must additionally achieve the following:- ·          Minimum of 4000 hours flying experience of which 2000 hours must be command on multi-engine  aircraft; Above 17 ton. ·          Group 1 endorsement on DASH 8 or Equivalent with a minimum of 500 hours command on type; ·          Pass an oral interview and flying acceptance check conducted by the Company; ·          Must pass a Base and Route check with an Instrument Rating within 10 and 70 hours respectively; ·          Track record of good performance as a Commander and no accident record. b) Duties and responsibilities : ·      

Job Vacancy At Precision Air - Cabin Crews (10-Posts)

                                                                                                                  JOB VACANCY Precision Air Services Plc is a fast growing private Tanzanian airline which operates in Partnership with Kenya Airways, with its strategies to expand wings beyond East Africa and Africa. In order to keep our services at a higher level and meet our customers’ maximum satisfaction We wish to invite applications from suitably qualified candidates to fill in this challenging position. POSITION:           CABIN CREWS(10-POSTS) REPORTS TO:     CHIEF CABIN CREW DUTY STATION: DAR ES SALAAM                            ROLE PURPOSE OF THE STATEMENT You will be reporting to Chief Cabin Crew/Assistants Chief Cabin Crew - Precision Air Services PLC. Please take note of your responsibilities. Consistently give quality customer service to passengers in a safe environment for their comfort and satisfaction KEY ACCOUNTABILITIE