Huko Bungeni mjini Dodoma, kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC), imewasilisha taarifa yake ya mwisho katika Bunge la kumi. Miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni taarifa maalumu kuhusu kampuni ya ndege ya Tanzania (ATCL). Ndege aina ya Airbus 320 iliyokuwa imekodiwa na ATCL kutoka kampuni ya Wallis Trading Inc. kwa Malipo ya USD 370,000 kila mwezi. Akiwasilisha taarifa hiyo, mwanyekiti wa kamati hiyo ndugu Zitto Kabwe alisema: "Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100. 2.8.1 Hali halisi ya ATCL kwa sasa Mheshimiwa Spika, kwa
Welcome to Aviation Tanzania! This is Tanzania's first aviation blog with over eight years now since its creation. Here you will find news and information related to aviation and hospitality industry. News and information covered here is collected from various sources globally.