Skip to main content

TAARIFA MAALUM YA PAC KUHUSU KAMPUNI YA NDEGE YA TANZANIA (ATCL)

Huko Bungeni mjini Dodoma, kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC), imewasilisha taarifa yake ya mwisho  katika Bunge la kumi. Miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni taarifa maalumu kuhusu kampuni ya ndege ya Tanzania (ATCL).

Ndege aina ya Airbus 320 iliyokuwa imekodiwa na ATCL kutoka kampuni ya Wallis Trading Inc. kwa Malipo ya USD 370,000 kila mwezi.

Akiwasilisha taarifa hiyo, mwanyekiti wa kamati hiyo ndugu Zitto Kabwe alisema:

"Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.

2.8.1 Hali halisi ya ATCL kwa sasa
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013 na kwa kuzingatia Taarifa ya Wizara ya Uchukuzi, imebainika kuwa ATCL kwa sasa ina Ndege moja tu aina ya Dash 8 – Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam huku ikiwa na madeni makubwa kama itakavyofafanuliwa hapo baadae.

2.8.2 ATCL imefikaje hapo ilipo kifedha na kuwa na Madeni makubwa?
Mheshimiwa Spika, baada ya kuvunjika kwa mkataba wa ubia baina ya SAA ana ATC, mnamo mwezi Machi 2008, Wizara ya Miundombinu kwa wakati huo iliingia katika makubaliano na Kampuni ya China Sonangol kuwa Kampuni hiyo ya China ingeleta ndege mpya 7 kwa ATCL ikiwamo Ndege 5 aina ya Airbus ambazo zingewasili mwaka 2012 na 2013.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Msajili wa Hazina na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, Wakati ATCL ikisubiri ndege hizo mpya, Kampuni ya China Sonangol iliitambulisha Kampuni ya Wallis Trading Inc kwa ATCL na kisha Kampuni hizi mbili (Wallis Trading Inc na ATCL) zikaingia mkataba wa Ukodishaji ndege aina ya Airbus 320 kwa kipindi cha miaka 6 kwa Malipo ya USD 370,000 kila mwezi.

Mheshimiwa Spika, huu ndio ulikuwa mwanzo wa mwisho wa ATCL, kwani baada ya Ndege hiyo kuwasili ilifanya kazi kwa muda wa miezi sita tu na baadae ilifungiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya usafiri wa anga. Ndege hiyo ilipelekwa kwa matengenezo makubwa mwezi Julai, 2009 nchini Ufaransa na haijawahi kurudi hadi leo wakati ambapo Serikali kama mdhamini wa ATCL anadaiwa fedha nyingi na Kampuni ya Wallis.

Mheshimiwa Spika, kutokana na deni la ATCL kwa Wallis linalofikia USD 42,459,316.12 hadi tarehe 31 Oktoba, 2011 na kufuatia majadiliano mbalimbali baina ya Serikali na Kampuni hiyo, Serikali imekwishalipa jumla ya USD 26,115,428.75 hadi sasa wakati bakaa inayodaiwa ni USD 23,996,327.82.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa sana na upotevu huu wa fedha za Umma ambao umetokana na mkataba mbovu ulioingiwa na watumishi wa Umma wasiokuwa waaminifu na uchungu na Taifa lao. Mabilioni ya fedha yanaoendelea kulipwa kwa Kampuni ya Wallis kwa huduma ya ndege iliyofanya kazi hapa nchini kwa miezi sita tu na kisha ndege hiyo kupelekwa Ufaransa kwa matengenezo ni fedheha kubwa kwa wazalendo wa Taifa letu. Aidha, Taarifa zinasema ndege hiyo ikiwa Ufaransa ilipakwa rangi na kukodishwa kwa Shirika la ndege la nchi ya Guinea wakati Serikali yetu ikiendelea kulipia tozo ya ukodishaji wa ndege husika.

Mheshimiwa Spika, ni wakati sasa kwa Serikali kuamua kwa dhati kushughulikia suala la ATCL kwa mapana yake ikiwa ni pamoja na kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis (ambalo lipo chini ya dhamana ya Serikali, hivyo ni fedha za Umma) ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL. Aidha, ni muhimu wahusika wa uingiaji wa mkataba husika wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke.

Mapendekezo kuhusu deni la USD 23,996,327.82 ambalo ATCL inadaiwa na Wallis Trading Inc.
KWA KUWA, Serikali haikunufaika na mkataba wa kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kwa Kampuni ya Wallis baada ya ndege hiyo kugundulika ni mbovu ndani ya miezi sita na kupelekwa kutengenezwa kwa muda mrefu,
NA KWA KUWA, Serikali inaendelea kulipa tozo ya ukodishaji wa ndege hiyo ambayo haifanyika kazi,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo;

a) Serikali kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL.


b) Serikali ihakikishe inawafikisha kwenye vyombo vya Sheria ili haki itendeke kwa wahusika wa uingiaji wa mkataba huo unaoendelea kuipa hasara Serikali kwani hadi sasa hakuna kesi iliyopelekwa mahakamani mahususi kwa waliongia mkataba husika."

Comments

  1. Jambo hili linaumiza sana. Kwa kweli mimi siamini hata kidogo kuwa, nchi yangu Tanzania eti imeshindwa kabisa kuwa na shirika la ndege zuri na lenye nguvu kabisa. Ama hakika twahitaji mabadiliko ya hali ya juu kwa hali hii.

    ReplyDelete

Post a Comment

Most Viewed Posts

Job Opportunities at Air Tanzania (ATCL)

VACANCIES ANNOUNCEMENT Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet. The Company is therefore inviting applications from qualified personnel to fill various positions. 1.      POSITIONS:  1.1. Dash 8 – Q400 Mechanical and Avionics Certifying Engineers (6 POSTS)     a)    Qualifications·         ·          Must possess a valid Aircraft Maintenance Engineers License (ICAO TYPE II).  ·         ·          Must possess a valid Dash 8 – Q400 Approval/License. ·      Must have successfully completed Dash 8 – Q400 type course from an Approved Training Organisation.        ·       Must have Aircraft Maintenance working experience, as a certifying engineer, of not less than 5 years; 2 of which being on Dash 8 – Q400. Experience must include release to service certification after “A” Check and above.        ·          Computer literacy·         ·          Fluency in English·        

Job Opportunities at Air Tanzania: Pilots-in-Command, Co-Pilots,Aircraft Maintenance Engineers and Cabin Crews.

Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet. The Company is therefore inviting application from qualified personnel to fill various positions. 1. POSITIONS: 1.1  Pilot-in-Command – Dash 8 (11 Posts) a) Qualifications: Must possess Airline Transport Pilot License (ATPL) and with performance “A”.Must additionally achieve the following:- ·          Minimum of 4000 hours flying experience of which 2000 hours must be command on multi-engine  aircraft; Above 17 ton. ·          Group 1 endorsement on DASH 8 or Equivalent with a minimum of 500 hours command on type; ·          Pass an oral interview and flying acceptance check conducted by the Company; ·          Must pass a Base and Route check with an Instrument Rating within 10 and 70 hours respectively; ·          Track record of good performance as a Commander and no accident record. b) Duties and responsibilities : ·      

Job Vacancy At Precision Air - Cabin Crews (10-Posts)

                                                                                                                  JOB VACANCY Precision Air Services Plc is a fast growing private Tanzanian airline which operates in Partnership with Kenya Airways, with its strategies to expand wings beyond East Africa and Africa. In order to keep our services at a higher level and meet our customers’ maximum satisfaction We wish to invite applications from suitably qualified candidates to fill in this challenging position. POSITION:           CABIN CREWS(10-POSTS) REPORTS TO:     CHIEF CABIN CREW DUTY STATION: DAR ES SALAAM                            ROLE PURPOSE OF THE STATEMENT You will be reporting to Chief Cabin Crew/Assistants Chief Cabin Crew - Precision Air Services PLC. Please take note of your responsibilities. Consistently give quality customer service to passengers in a safe environment for their comfort and satisfaction KEY ACCOUNTABILITIE