Kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania ikilinganishwa na thamani ya dola ya Kimarekani ni miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia kudumaa na kufa kwa mashirika au kampuni za ndege za hapa Tanzania. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mtandao wa aviationtz, ambao umehusisha wataalamu wa sekta ya usafiri wa anga, imeonekana kuwa pamoja na sababu nyingine zikiwemo za uendeshaji mbaya wa mashirika, mtaji mdogo na pia ushindani mkubwa katika soko lenye wateja wachache, kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania ni sababu nyingine kubwa ya mashirika mengi hasa yale makubwa kutokufanya vyema katika biashara. Athari ya shilingi inaonekana kutokana na ukweli kwamba mauzo ya tiketi au tozo za nauli kwa safari za ndani ya Tanzania hufanywa kwa kutumia shilingi. Kwa hiyo pato la makampuni ya ndege linakusanywa katika shilingi. Kwa upande wa matumizi na kulipia huduma mbalimbali mashirika haya hutakiwa kulipa kwa dola ya kimarekani au Euro. Matengenezo yote ya ndege na ununuzi wa
Welcome to Aviation Tanzania! This is Tanzania's first aviation blog with over eight years now since its creation. Here you will find news and information related to aviation and hospitality industry. News and information covered here is collected from various sources globally.