Ifuatayo ni sehemu ya bajeti ya wizara ya uchukuzi kwa upande wa usafiri na uchukuzi kwa njia ya anga kwa mwaka 2015/2016 kama ilivyowasilishwa na waziri Samueli Sitta katika bunge la bajeti mjini Dodoma. 4.0 USAFIRI NA UCHUKUZI KWA NJIA YA ANGA 4.1 Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga 90. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeendelea kuhakikisha kuwa viwanja vya ndege na huduma za usafiri wa anga nchini vinakidhi masharti na kanuni zilizowekwa. Ili kuhakikisha kuwa kanuni hizo zinazingatiwa, katika mwaka 2014/2015, viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Abeid Amani Karume na Kilimanjaro (KIA) vilikaguliwa na kupata vyeti vya ubora kulingana na matakwa ya vigezo vya Kimataifa ya viwanja vya ndege. Aidha, viwanja vya ndege vya Arusha, Mwanza, Kigoma, Tabora, Bukoba, Mtwara, Tanga, Lindi na Iringa pia vilikaguliwa na kupewa vyeti vya ubora. Utekelezaji wa uboreshaji wa viwanja vya ndege nchini ni mzuri kiwango cha
Welcome to Aviation Tanzania! This is Tanzania's first aviation blog with over eight years now since its creation. Here you will find news and information related to aviation and hospitality industry. News and information covered here is collected from various sources globally.