Ndege mpya DHC-8-402Q, MSN 4495, ya shirika la ndege la Air Tanzania, tayari imeshakamilika kupigwa rangi na ipo katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza safari yake ya kuja nchini Tanzania. Ndege hii ambayo kwa sasa ina usajili wa C-FIFG (usajili wa majaribio, Canada) ni ya kwanza kati ya ndege mbili za aina ya Bombadier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya shirika la ndege la ATCL ambapo zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi wa septemba mwaka huu. Muonekano wa sasa wa ndege hiyo ikiwa katika rangi za shirika la ndege la Air Tanzania. Picha kwa hisani ya Jetstream. Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mitandao mbalimbali, ndege hii ni mpya, imetengenezwa mwaka 2015, namba yake ya kutengenezwa (MSN) ni 4495. Kwa sasa ina umri wa mwaka mmoja na miezi minne. Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionesha ndege hiyo ikiwa na rangi nyeupe, wakati ikifanyiwa majaribio kabla ya kuuzwa kwa serikali ya Tanzania. Picha hii imepigwa 22
Welcome to Aviation Tanzania! This is Tanzania's first aviation blog with over eight years now since its creation. Here you will find news and information related to aviation and hospitality industry. News and information covered here is collected from various sources globally.