ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

Ndege mpya DHC-8-402Q, MSN 4495, ya shirika la ndege la Air Tanzania, tayari imeshakamilika kupigwa rangi na ipo katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza safari yake ya kuja nchini Tanzania. 

Ndege hii ambayo kwa sasa ina usajili wa C-FIFG (usajili wa majaribio, Canada) ni ya kwanza kati ya ndege mbili za aina ya Bombadier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya shirika la ndege la ATCL ambapo zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi wa septemba mwaka huu.

    Muonekano wa sasa wa ndege hiyo ikiwa katika rangi za shirika la ndege la Air Tanzania. Picha kwa hisani ya Jetstream.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mitandao mbalimbali, ndege hii ni mpya, imetengenezwa mwaka 2015, namba yake ya kutengenezwa (MSN) ni 4495. Kwa sasa ina umri wa mwaka mmoja na miezi minne.


Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionesha ndege hiyo ikiwa na rangi nyeupe, wakati ikifanyiwa majaribio kabla ya kuuzwa kwa serikali ya Tanzania.

Picha hii imepigwa 22 Mei 2016, huko Downsview (CYZD), Toronto, Canada. Picha kwa hisani: Nigel Harris.
Picha hii imepigwa 22 Mei 2016, huko Downsview (CYZD), Toronto, Canada. Picha kwa hisani: Nigel Harris.


 Picha hii ilipigwa huko Downsview, tarehe 29-Apr-2016, ikiwa katika rangi yake nyeupe, ikimilikiwa na mtengenezaji, kampuni ya Bombardier Inc. Montreal, QC. 
Picha na: Kenneth I. Swartz.About aviationtz

https://plus.google.com/+AviationTanzania/about.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

2 comments:

 1. Naitwa victus,napenda sana link yenu ya Facebook.inatusaidia sana kupata habari za aviation.
  Niko kwenye aviation industry.
  Thank you

  ReplyDelete
  Replies
  1. Asante sana ndugu Kili Temba, tunapata faraja kusikia hivyo, tafadhali endelea kutufuatilia kwa habari zaidi za uhakika katika sekta hii ya usafiri wa anga.

   Delete


Top