Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

Fastjet yajiandaa kupokea ndege yake,ATR72-600.

Shirika la ndege la fastjet linatarajia kupokea ndege yake aina ya ATR72-600 hivi karibuni. Kwa mujibu wa mtandao wa Skyliner Aviation, ndege hiyo inaonekana ikiwa tayari imeshapakwa rangi za fastjet, na taarifa zinasema inatarajiwa kusajiliwa Tanzania na kuanza kazi katika mwezi wa januari 2018. Fastjet wanasema ATR itawawezesha kutua katika maeneo ambayo ndege aina ya jet haziwezi kutua. Kwa maana hiyo sasa fastjet wataweza kutua katika viwanja kama vile Mtwara, Kigoma, Tabora, Arusha na kwingine kule ambapo ATR72 inaweza kutua kwa usalama. Picha kwa hisani ya mtandao wa Skyliner. Ndege za ATR si ngeni hapa nchini kwani shirika la ndege la Precision Air linamiliki kiasi kikubwa cha ndege hizo, takribani ndege 9 zikiwa ni ATR72 na ATR42, na ni miongoni mwa mashirika yanayo ongoza barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya ATR, na pia ina karakana yake ya ufundi ambayo imebobea katika ufundi na matengenezo ya ndege hizi za ATR. ATR72 ina uwezo wa kubeba abiri kati ya