Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2019

SWISS yasimamisha ndege zake zote za Airbus A220 kupisha ukaguzi wa injini.

Shirika la ndege la SWISS Inrernational Airlines ambalo linamilikiwa na Shirika la ndege la Lufthansa la Ujerumani, limesimamisha safari za ndege zake zote aina ya Airbus A220 kutokana na matatizo ya injini zake. Injini zote za ndege hizo zimelazimika kukaguliwa ili kuhakiki usalama wake. Ndege hizo hutumia injini aina ya PW 1500G zinazotengenezwa na kampuni ya Pratt & Whitney ya Canada.  Shirika hilo limesema lipo katika mazungumzo na mamlaka za usimamizi wa usafiri wa anga na pia mtengenezaji wa ndege hizo ambaye ni kampuni ya Airbus.  Mamlaka ya usafiri wa anga ya Marrekani FAA ilitoa muongozo kwamba injini zote za A220 ambazo ni Pratt & Whitney zinatakiwa kufanyiwa ukaguzi zaidi wa kiusalama.  Kusimamishwa kwa ndege hizo kunatokana na matatizo ya kiufundi ya mara kwa mara ya injini hizo. Mnamo July 25 vipande vya injini ya A220 vilikatikakatika na kuanguka katika anga la Paris, ndege hiyo ikiwa safarini kutokea Geneva kwenda London.Tukio kama hilo linarip