Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

Kenya Airways (KQ) yabadili ndege ya abiria "Dreamliner" kubebea mizigo

Katika hali ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi na kuendelea kupambana kwenye biashara katika kipindi hiki cha janga la #COVID-19, shirika la ndege la Kenya, Kenya airways limekuja na ubunifu wa kutumia ndege zake za dreamliners kubeba na kusafirisha mizigo. Mizigo inayosafirishwa ni misaada ya madawa na vifaa tiba na pia vyakula na mbogamboga. Mizigo hiyo husafirishwa baina ya Kenya na nchi nyingine. Ndege ya kwanza ya mizigo ilikuwa ni ya madawa na vifaa tiba iliyoondoka Nairobi kuelekea Johannesburg, Afrika ya Kusini. Ndege ya pili ya mizigo ilibeba mazao ya shambani, mbogamboga kutoka Nairobi ikielekea London Uingereza. Ndege ya tatu ilikuwa ni ya madawa na vifaa tiba kutoka China kwenda Kenya vikiwa ni katika jitihada za kupambana na janga la #COVID-19. Kwa kawaida ndege hizi za dreamliner hubeba abiria. Lakini kufuatia kipindi hiki cha janga la  COVID19 mashirika ya ndege yamelazimika kusitisha kutoa huduma za usafiri wa abiria kutokana na makatazo ya mat