Ndege aina ya Cessna 208B yenye usajili 5H-MZA yaanguka baharini huko Comoros ikiwa na watu 14 ndani yake. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la FLY ZANZIBAR LIMITED ikiwa imekodiwa na shirika la ndege la AB AVIATION la Comoro, ikifanya safari Y61103 kati ya kisiwa cha Moroni na Mohéli, ilianguka wakati ikielekea kutua katika uwanja wa Bander es Salaam Airport, Fomboni, Comoros – katika kisiwa cha Moheli. Shirika la ndege la AB Aviation lilitangaza kupotea kwa ndege hiyo iliyopaa kutoka Moroni saa tano na dk 50 na kupotea katika radar, baharini, umbali wa 2.5 km kutoka uwanja wa ndege wa Mohéli Juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea, mpaka sasa ni baadhi ya mabaki ya ndege tu ndio yamepatikana. Matumaini ya kupata abiria na marubani wakiwa hai yanazidi kufifia. Taarifa zinaeleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na hali mbaya ya hewa baharini katika maeneo ya visiwa vya comoro. Orodha ya majina ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo Baadhi ya mabaki ya ndge hiyo yakiwa yameok
Welcome to Aviation Tanzania! This is Tanzania's first aviation blog with over eight years now since its creation. Here you will find news and information related to aviation and hospitality industry. News and information covered here is collected from various sources globally.